Mwanamuziki wa Hiphop kutoka Tanzania Chemical amepata heshima ya kipekee kutoka Chuo kikuu cha St.Andrwes Scotland, kwenye chuo anachopata masomo yake ya ngazi ya juu ya elimu.
Katika makala hayo yaliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya chuo hicho imemuelezea rapa huyo katika mafanikio yake ya muziki na masomo huku wakimpongeza na kujivunia kuwa sehemu ya wanafunzi wao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Chemical ameandika ujumbe unaosomeka “Jamani eeeh… Naomba mninunulie kalambogini ka kutembelea huku chuoni. Nishakuwa maarufu mieee. Mpaka Uingereza sasa hivi wanajua kuhusu tuzo. What a better way to be acknowledged. Found myself in the University newsletter. Thank you for this recognition. Jamani hii kwangu ni tuzo nyingine,” –
Ikumbukwe Chemical alishinda tuzo za Tanzania Music Awards 2022 kama msanii bora wa kike wa HipHop wa mwaka nchini humo.