You are currently viewing Rapa Gabiro Mtu Necessary aingia kwenye hatua ya kujadiliwa (consideration ) Grammy

Rapa Gabiro Mtu Necessary aingia kwenye hatua ya kujadiliwa (consideration ) Grammy

Habari nzuri na kubwa kwa muziki wa Kenya ni kuwa kwa mara ya pili rapa Gabiro Mtu Necessary, amefanikiwa kuingia kwenye hatua ya kujadiliwa (consideration ) kwa ajili ya kuingia kuwania tuzo za 65 za Grammy .

Gabiro Mtu Necessary ameingia kwenye tuzo hiyo kupitia kipengele cha Best Global Music Album na album yake Saint John lakini pia kupitia kipengele cha Best Global Music Performance na wimbo wake wa Pok Alando.

Hata hivyo msanii huyo anaungana na baadhi ya wasanii wengine duniani kusubiri kura za mapendekezo kutoka Academy ya Grammy, na wakipitishwa basi wataingia moja kwa moja kuwania tuzo hizi zenye heshima kubwa ulimwenguni.

Utakumbuka mwaka wa 2021 alipata umaaarufu nchini baada ya EP yake iitwayo Jenesis kuingia kwenye hatua ya kujadiliwa kuwania tuzo za Grammy kama Best Global Music Album pamoja na wasanii wenzake Octopizzo na Victoria Kimani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke