Rapper kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju ameingia kwenye headlines mara baada ya kujikuta akimpiga teke shabiki yake kwenye moja ya performance yake wikiendi hii iliyopita.
Shabiki huyo alimwagia kinywaji dancer wake Trisha Woodz akiwa jukwaani akiwaburudisha mashabiki, kitendo ambacho kilimkasirisha Gravity Omutujju ambaye alihamua kurusha teke kwa shabiki aliyehusika na kitendo hicho huku akimtolea maneno makali.
Hata hivyo jambo hilo limezua mjadala mtandaoni ambapo baadhi ya watu wamehoji kuwa Gravity Omutujju alishusha brandy yake ya muziki kwa kitendo cha kumpiga teke shabiki yake huku wengine wakimuunga mkono kwa hatua ya kutaka kumuadhibu shabiki yake huyo.