You are currently viewing RAPA GRAVITY OMUTUJJU ATISHIA KUJITOA UHAI KISA MUZIKI

RAPA GRAVITY OMUTUJJU ATISHIA KUJITOA UHAI KISA MUZIKI

Rapa kutoka Uganda Gravity Omutujju ametoa wito kwa Rais Yoweri Museveni kutofunga tena uchumi wa taifa hilo kutokana na Corona.

Rapa huyo ametishia kujitoa uhai kama rais wa Uganda Yoweri Museveni atasitisha tena matamasha ya muziki mara baada ya kufungwa kwa kipindi cha miaka miwili.

Omutujju amesema ana mpango wa kuandaa shoo katika eneo la Cricket Oval jijini Kampala mwezi Februari mwaka huu ili aweze kupata pesa za kulipa madeni ambayo aliyapata kipindi cha Corona

Kauli ya Omutujju imekuja mara baada ya rais Yoweri Museveni kutangaza kufungua tasnia ya muziki nchini humo tarehe 24 mwezi huu baada ya kusitishwa  kutokana na katazo la kuzuia msambao wa Corona.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke