Video imevuja ikimuonesha rapa Gunna akikiri makosa yake mahakamani siku ya jana ambapo ameonekana akikubali kuwa “YSL” ni kundi la kihalifu. Wengi wamedai kuwa amewasaliti wenzake kwa kufikia maamuzi hayo ili tu aachiwe huru na msala uendelee kubaki kwa wenzie.
Gunna aliachiwa jana kutoka jela ambapo alikaa kwa muda wa miezi 7 jela. Rapa huyo na wanachama wenzake wa YSL akiwemo Young Thug walishtakiwa kwa makosa ya kukiuka sheria inayopambana na rushwa lakini pia vitendo vya kihalifu mtaani.
Hata hivyo wanachama wengine wa lebo ya muziki ya YSL wataendelea kubaki gerezani mpaka pale kesi yao itakapoanza kusikilizwa.