Rapa kutoka Kenya Juliani amekanusha kuteuliwa kama afisa mkuu wa masuala ya burudani katika muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja.
Kupitia taarifa yake kwenye mitandao yake ya kijamii Juliani amesema madai yanayosambaa mtandaoni kuhusu kuteuliwa kwake hayana ukweli wowote kwa kuwa hajapokea taarifa yeyote kutoka kwa uongozi wa azimio la umoja kuhusu suala la yeye kupewa kazi.
Hitmaker huyo wa “Utawala” amesema hajaajiriwa na hana uhusiano wowote na chama chochote cha kisiasa nchini huku akisema ikitokea ameshirikiana na mrengo wowote wa kisiasa ataweka wazi kwa mashabiki wake.
Hata hivyo amewataka wakenya kufanya maamuzi ya busara kwa kuwachagua viongozi watakaoleta maendeleo kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu badala ya kudanganywa na wanasiasa wasio kuwa na maono.
Kauli ya Juliani imekuja mara baada ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kudai sababu za afred mutua kukimbia muungano wa azimio ni kutokana na rapa huyo kupewa wadhfa wa afisa mkuu wa masuala ya buradani ikizingatiwa kuwa mwaka jana rapa huyo aliripotiwa kumpokonya gavana huyo mke wake.