Rapa Kanye West ni kama bado anatamani kurudiana na baby mama wake Kim Kardashian kwa sababu anazidi kuja na matukio mbalimbali kila kukicha.
Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram rapa huyo ameshare picha ya watoto wake wakiwa pamoja na mama yao, Kim Kardashian na kuandika kuwa mungu asaidie familia yake irudi kuwa pamoja.
Baada ya Kanye West kuonesha kuwa bado anatamani familia yake irudi kama zamani, mpenzi wa sasa wa Kanye West, Julia Fox anasema hana wasiwasi kwa sababu anachojua kwa sasa Kanye West ni wa kwake na anajua kuwa bado ana mabaki ya hisia kwa mrembo Kim kardashian ila yeye anachukulia ni hali ya kibinadamu kumkumbuka ulietengana nae.
Siku kadhaa zilizopita tuliona kupitia mitandao ya kijamii kanye west akimchana baby mama wake Kim kwa mambo mbalimbali ikiwemo kumuunganisha mtoto wao North West kwenye mtandao wa Tiktok bila idhini yake.