You are currently viewing RAPA KHALIGRAPH JONES AACHIA RASMI “INVISIBLE CURRENCY” ALBUM

RAPA KHALIGRAPH JONES AACHIA RASMI “INVISIBLE CURRENCY” ALBUM

Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Khalighraph Jones ameachia rasmi albamu yake mpya kutoka studio “Invisible Currency” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

Invisible Currency ina ina jumla ya nyimbo 17 za moto huku ikiwa na collabo 10 pekee kutoka kwa wakali kama Ali kiba, Juma Jux, Rude Boy, Dax, Mejja, Scar, Adasa na wengine wengi.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Papa Jones ametoa shukran kwa watu wote waliofanikisha mchakato wa kuiandaa album yake mpya ambapo amewataka mashabiki zake kuifutilia album ya Invisible Currency kwenye mtandao wa kustream muziki wa Boomplay Kenya.

Invisible Currency inakuwa album ya pili kwa mtu mzima Khaligraph Jones  baada ya “Testimony 1990” ya  mwaka 2018 iliyokuwa na jumla ya ngoma 17.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke