Rapa kutoka nchini Kenya Khaligraph Jones amefunguka mpango wa kuachana muziki wa Hiphop na kuanza kuimba muziki wa injili.
Kwenye mahojiano na Plug tv Khaligraph amesema kwamba amekuwa na ndoto ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili toka utotoni, hivyo anasubiri muda mwafaka kufika ili aweze kueneza injili kupitia muziki wake kwani hata kabla ya kuanza kufanya muziki wa kidunia alikuwa msanii wa nyimbo za injili.
Mbali na hayo Boss huyo wa Blue Ink ameweka wazi sababu za kutocheza kimahaba na wanawake akiwa anatoa burudani jukwaani kama namna wasanii wengine wamekuwa wakifanya.
Papa Jones amesema brand au chapa yake ya muziki haimruhusu kufanya vitu kama hivyo ikizingatiwa pia ana familia.