You are currently viewing Rapa Khaligraph Jones akerwa na abiria wanaotumia vyoo vya ndege kwenda haja kubwa

Rapa Khaligraph Jones akerwa na abiria wanaotumia vyoo vya ndege kwenda haja kubwa

Rapper Khaligraph Jones amesikitishwa na watu wanaopenda kujisaidia ndani ya vyoo vya ndege wakati wa safari za ndani ya nchi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Papa Jones amesema sio jambo la busara kwa watu kwenda haja kubwa kwenye vyoo vya ndege kwa kuwa inaharibia hali ya hewa.

Hitmaker huyo “Kamnyweso” ameshauri watu wajenge tamaduni za kuvumilia wakati wa safari za ndani hadi ndege itakapotua kwa kuwa jambo hilo linakera mno.

Hata hivyo amedai ndege ambayo alikuwa ameabiri ilikuwa inanuka kinyesi cha mtu baada ya abiria mmoja kutumia vyoo vya ndani.

“Nashangaa sana na watu wanaenda kwa choo ya ndege kukunia na saa hizo ni a 40-minute flight. Shikilia hiyo kitu mpaka tuland bwana, ndege imenuka pupu leo,” Aliandika Instagram.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke