You are currently viewing RAPA KING KAKA ALAMBA SHAVU YA KUWA BALOZI WA KIMATAIFA WA SPORTS BET

RAPA KING KAKA ALAMBA SHAVU YA KUWA BALOZI WA KIMATAIFA WA SPORTS BET

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportsbet.io imemtangaza Rapa King Kaka kuwa balozi wake mpya wa kimataifa.

Katika taarifa Sportsbet.io imesema wamemchagua King Kaka kwa sababu rapa huyo anaendana na vigezo vya kampuni hiyo kwani ana uwezo mkubwa wa kuwafikishia vijana wengi ujumbe wa kuwekeza na sportsbet.io

Akitangaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia mitandao yake ya kijamii King Kaka amesema ameweka historia ya kuwa mwaafrika wa kwanza kuwa balozi wa kimataifa wa Sportsbet.io huku akisema kwamba kampuni hiyo italeta mwamko mpya kwenye soko la michezo ya kubashiri Barani Afrika.

King Kaka ambaye ni moja kati ya marapa wakali Afrika anatarajiwa kutumia ubunifu na umaarufu wake kuwashawishi wafuasi wake kushiriki kwenye mchezo wa kubashiri kupitia mtandai wa sportsbet.io kama njia ya kujikwamua kiuchumi.

Utakumbuka Sportsbet.io ni kampuni ya michezo ya kubashiri kwa kutumia sarafu ya mtandaoni ya Crypto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke