You are currently viewing Rapa King Kaka atangaza kuachia Album yake mpya Disemba 2022

Rapa King Kaka atangaza kuachia Album yake mpya Disemba 2022

Rapa kutoka nchini Kenya King Kaka ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo ameipa jina la 2nd life kabla mwaka huu 2022 haujaisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bosi huyo wa Kaka Empire amesema ameamua kuja na album hiyo kwa ajili ya kumrudishia Mwenyezi Mungu fadhila kwa kumpa nafasi nyingine ya kuishi duniani ikizingatiwa kuwa mwaka 2021 nusra ampoteze maisha yake baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana uliofanya kupoteza uzani wa kilo 33.

Hitmaker huyo wa Diana amesema album ambayo ni ya tano katika safari yake ya muziki itaingia sokoni Disemba 24 mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju 17 ya moto.

“One promise I made was to give gratitude, something we often take for granted. Inspired by what I’ve been through I am officially announcing my next body of work , my 5th album Titled #2ndLife that drops this 24th December.”

Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa tayari amekamilisha video za nyimbo ambazo zinapatikana kwenye album yake ya 2nd Life, na ataachia rasmi video ya kwanza Novemba 20 mwaka huu huku akiwashukuru mashabiki kwa upendo ambao wamekuwa wakimuonyesha kwa miaka mingi.

“I am excited , genuinely excited. 17 Music Videos!! Weuh 17! The journey begins. We release the 1st one this 20th. Asanteni for loving me over the many years.”,

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke