Rapa kutoka nchini Kenya Boutross ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la Mawingu.
Album hiyo yenye jumla ya nyimbo 9 za moto, ina kolabo 7 kutoka kwa wakali kama Trio Mio, Maandy, Juice Man, Young Kith, Savage, na Beevlings.
Mawingu Album kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani na ina ngoma kama Dapa Dapa, Can’t Wait, Ithaa, Demand na nyingine nyingine.
Hii ni Album ya tatu kwa mtu mzima Boutross tangu aanze safari yake ya muziki baada ya “Kabla ya Mtindo” iliyotoka mapema mwaka wa 2022 ikiwa na jumla ya mikwaju 8 ya moto.