Rapper Femi One ameshinda kipengele cha rapper bora Afrika kwenye tuzo za Afrimma 2022 zilizokamilika wikiendi iliyopita huko Dallas nchini Marekani.
Femi one ametumia mitandao yake ya kijamii kusherekea mafanikio kwa kushukuru uongozi wake pamoja na mashabiki kwa kumshika mkono kwenye safari yake ya muziki huku akiwahimizi marapa wa kike chipukizi kutia bidii katika kazi zao kwa kuwa wana nafasi zao kwenye tasnia ya muziki.
“WE WON!!! Best Female Rapper In Africa . The first East African Female rapper to take it home , it’s such a big pat on the back for my team and I for all the work we’ve put in throughout the years . Truly consistency, patiency pays !!”
“This should be an encouragement for all the up and coming Female rappers! There is a spot for you in this industry, keep building , keep doing it , they are watching . Thank you all so much for the continued support”, Aliandika.
Femi one ambaye ni msanii wa kwanza wa kike kushinda tuzo ya Afrimma kwa upande wa muziki wa Hiphop anajiunga na Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na Zuchu ambao walishinda tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika mashariki, Best Live Act na msanii Bora wa kike Afrika Mashariki mtawalia.
Femo One hakuwa Mkenya pekee aliyeteuliwa kuwania tuzo hizo, wengine ni pamoja na Khaligraph Jones- (Best Male East Africa), Otile Brown- (Best Male East Africa), Jovial- (Best Female East Africa), (Ssaru- Best Newcomer), Sauti Sol- (Best Live Act), na Fena Gitu- (Best Female Rap Act).