Rapa kutoka nchini Kenya Octopizzo ameachia rasmi album yake mpya inayokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
Album hiyo inayokwenda kwa jina la Lamu Nights ina jumla ya ngoma 10 za moto ambazo amewashirikisha wakali kama Wendy Kay, Jivu, Tito Wagithomo, Coaster Ojwang, Okella Max na Burklyn Boyz.
Album hiyo ina nyimbo kama No Signal, Bad Vibes, Want It, Vacation, Moaning, Achupa na na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa Youtube.
Lamu Nights ni Album ya saba kwa mtu mzima Octipozzo, baada ya Fuego iliyotoka mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 12 ya moto.