You are currently viewing RAPA KUTOKA MAREKANI MYSTIKAL ATUPWA JELA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

RAPA KUTOKA MAREKANI MYSTIKAL ATUPWA JELA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

Rapa Mystikal amekamatwa na sasa anashikiliwa katika Jela ya Ascension Parish mjini Louisiana ambapo amefunguliwa mashtaka kadhaa ikiwemo ubakaji, unyanyasaji majumbani, kumshikilia mtu ndani bila ridhaa yake na makosa mengine.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 51 aliwahi kutamba na ngoma zake kama “It Ain’t My Fault” na “Shake Ya A***” Hii sio mara ya kwanza kukutwa na makosa hayo, tangu mwaka 2003 Mystikal amekuwa akituhumiwa, 2004 alifungwa miaka 6 Jela kwa kumshambulia kingono hairstylist wake.

Utakumbuka Mwaka 2017 pia alifunguliwa mashtaka ya ubakaji. 2019 aliachiwa baada ya kulipa dhamana ya zaidi ya TSh. Bilioni 7, mwaka 2020 mashtaka hayo yalifutwa kufuatia kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke