Rapa Meek Mill ametangaza kuachana na mtandao wa Twitter baada ya kuweka wazi rasmi kuifuta akaunti yake ya mtandao huo.
Sababu kubwa hasa ya Meek Mill kufikia maamuzi hayo amebainisha kuwa, mtandao huo una utaratibu na watu wa ajabu mno na sasa atakuwa akiutumia zaidi mtandao wa YouTube.
“Nimeamua kuiondoa akaunti yangu ya Twitter jumla na nitatumia mitandao mingine ya kijamii yenye hali nzuri ikiwa na lengo la kujenga, na hata kutia motisha. Kwa hiki ambacho kinaendelea upande wa Twitter kimepelekea nichukue maamuzi hayo.” Unasomeka ujumbe wa Meek Mill kabla hajaifuta akaunti yake hiyo.
“Nitakuwa nikitumia akaunti yangu ya YouTube badala ya Twitter kwa ajili ya kuendelea kuwa karibu na watu wangu”, Alitweet Meek Mill.