Member wa kundi la Nannoma ambalo lilianza muziki mwaka wa 1999 na kujipata umaarufu kwenye tasnia ya muziki nchini kupitia singo iitwayo Kila Saa, msanii Big Mike, amefariki dunia oktoba 17 mwaka huu.
Big mike alikuwa rapa na mtayarishaji mashuhuri wa muziki, wakati muziki wa kisasi kipya nchini Kenya ulikuwa kwenye hatua za mwanzo kukua, enzi ambayo kulikuwa na makundi machache ya muziki wa hiphop.
Kabla ya umauti kumkuta, Big mike alikuwa anajishughulisha na masuala ya kuzalisha kazi za wasanii na kipindi cha uhai wake alipata fursa ya kufanya kazi na wasanii tajika nchini akiwemo Abass kubaff, wyre na wengine wengi.
Big Mike atakumbukwa kwenye kiwanda cha muziki nchini kama muasisi wa mashindano ya kurap ya Wapi Rap Battles ambayo yalikuwa yanawapa wasanii chipukizi nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kupitia muziki wa hiphop.