You are currently viewing RAPA NAS NA KAMPUNI YA GOOGLE WAWEKEZA MABILLIONI YA PESA NIGERIA

RAPA NAS NA KAMPUNI YA GOOGLE WAWEKEZA MABILLIONI YA PESA NIGERIA

Rapa wa Marekani Nas akishirikiana na kampuni ya Google wamewekeza kiasi cha shillingi billioni 2.3 za Kenya kwenye kampuni ya Kiafrika iitwayo Carry1st ambayo inahusika na kutengeneza Mobile Games.

Kwa mujibu wa The Hollywood Reporter, kiasi hicho cha fedha kitakwenda kusaidia kampuni hiyo kutanua wigo wa maudhui na pia kusaidia timu ya Wahandisi (engeeners)

CEO na mwanzilishi wa Carry1st Bwana Cordel Robbin-Coker amesema wawekezaji hao wapya sio tu wameleta ahueni upande wa fedha lakini pia wameongeza kiwango cha maarifa kwa kuleta wataalamu ambao watasaidia kampuni hiyo kukua.

Kampuni ya Carryfirst ina makazi yake nchini Nigeria.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke