Female Rapper kutoka Kenya Sylvia Ssaru ametangaza ujio wa kolabo yake na mwanamuziki wa Bongofleva Darassa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ssaru ame-share picha ya pamoja akiwa na bosi huyo wa lebo ya muziki ya Classic Music Group ambapo amethibitisha kuwa mashabiki wategemee kazi mpya kutoka kwao.
Duru za kuamiinika zinasema Wawili hao wanafanya wimbo huo chini ya maprodyuza Motif D Don kwa ushirikiano wa Vicky Pon Dis ambao mara kwa mara wamekuwa wakifanya kazi na Sylvia Ssarru.
Wimbo huo utakuwa wa nne kwa Darassa kufanya na wasanii wakenya kwani tayari ana wimbo wa pamoja na Nameless, Jovial, Hart The Band pamoja na Femi One.
Ikumbukwe Sylvia Saru kwa sasa yupo kwenye maandalizi ya album yake mpya ambayo alituahidi kuwa ana mpango wa kuachia ndani ya mwaka wa 2022.