Rapa Tory Lanez ameachiwa huru kutoka rumande baada kufanikiwa kulipa dhamana ya shilling milllioni 40 za Kenya.
Aprili 5 mwaka huu zilitoka taarifa za mkali huyo kutoka nchini Canada kupigwa pingu na kuweka rumande ya mahakama mjini Los Angeles baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka amri ya mahakama iliyotolewa kumkinga Megan Thee stallion kwenye shtaka lao linaloendelea.
Ikumbukwe Tory Lanez anakabiliwa na Mashtaka mawili ambayo ni kumshambulia rapa Megan thee Stallion mwaka 2020 na pia kubeba silaha yenye risasi kinyume na sheria.