Staa wa muziki kutoka Marekani Travis Scott ameendelea kudokeza kuhusu ujio wa album yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia hivi karibuni.
Aprili 11 mashabiki wa mkali huyo walipagawa mara baada ya kuona mabango (Billboards) yenye ujumbe kuhusu album hiyo kwenye barabara za Jiji la California, Marekani.
Hii itakuwa Album yake ya Nne ikiifuata ‘Astroworld’ ya mwaka 2018.