Rapa Wakazi amefunguka kuhusu hali ya muziki wa Hip Hop kwa sasa nchini Tanzania.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Wakazi amesema wasanii wa Hip Hop wamepoteza mvuto wa kibiashara, hivyo ni ngumu kwa wawekezaji kuwadhamini.
Wakazi amefunguka hayo wakati akijibu tweet ya mdau mmoja ambaye alitoa pendekezo kwamba, anatamani kufanyika kwa onesho moja kubwa la Hip Hop mwezi huu.
Wakazi ambaye amekuwa akipaza sauti na kutoa mitazamo yake kwenye mambo mbali mbali, ameongeza kwamba hata kampuni moja ya bia ambayo imekuwa ikiupa nguvu muziki wa Hip Hop, mwaka huu wamehamia kwa Ma-DJ na sio wasanii wa Hip Hop kutokana na kukosa weledi na uwezo wa Kibiashara nyuma ya wasanii wa Singeli na Bongo fleva.