You are currently viewing RAPA WANGECHI ADOKEZA UJIO WA ALBUM MPYA YA SCAR MKADINALI

RAPA WANGECHI ADOKEZA UJIO WA ALBUM MPYA YA SCAR MKADINALI

Rapa wa kike nchini Wangechi amedokeza kuwa member wa  kundi la Wakadinali, Scar Mkadinali ana mpango wa kuachia album yake mpya mwisho mwa mwezi huu wa Januari.

Wangechi amethibitisha hilo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram kwa kusema kwamba  album ya rapa huyo iitwayo Easy itaingia sokoni januari  24 mwaka huu.

Hata hivyo hajaweka wazi idadi ya ngoma ambazo zitapatikana kwenye album hiyo ila Wangechi atakuwa moja kati ya wasanii ambao watashirikishwa kwenye album ya Scar Mkadinali.

Ikumbukwe mwaka wa 2019 Wangechi na Scar Mkadinali waliachia singo yao ya pamoja inayokwenda kwa jina la Sana Sana.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke