Rapa kutoka marekani Young Dolph ameuawa kwa kupigwa risasi nje ya duka mjini Memphis. Rapa huyo mwenye umri wa miaka 36 ameuawa akiwa anatoka kwenye duka hilo kununua cookies.
Mmiliki wa duka hilo amesema mtu mmoja alitokea na gari kisha kumchapa risasi Dolph mchana wa saa saba Novemba 17 mwaka huu wa 2021. Tovuti ya FOX13 imeripoti kwamba umati watu ulijitokeza eneo hilo na kulala chini huku vilio vikitawala
Ikumbukwe Young Dolph alipata umaarufu nchini Marekani Mwaka wa 2016 alipoachia album yake ya kwanza, iitwayo King of Memphis. Wakati wa uhai wake Young Dolph alifanikiwa kufanya jumla ya album 7, mixtapes 19 na EP 2.