Rapa kutoka Tanzania Rapcha ametangaza kuwabariki mashabiki zake na EP yenye jumla ya nyimbo 5
EP hiyo ambayo ameipa jina la “TO THE TOP” itaingia sokoni rasmi Ijumaa hii, Mei 20.
Kwenye ujio huu mpya, “To The Top” rapcha amewashirikisha wasanii kama Frida Amani na Baraka The Prince kwenye wimbo namba 4,uitwao Melody na wimbo namba 5 uitwao Bado, zikiwa ndio collabo pekee. Nyimbo nyingine ni pamoja na Suu, Interview na Wait.
Huu ni muendelezo wa nyota huyo wa rap nchini kuendelea kukata kiu ya mashabiki wake wakiwa wanaendelea kusubiria album yake ya pili baada ya ‘Wanangu 99’ iliyotoka Septemba mwaka jana.