You are currently viewing RAPPER BARACK JACUZZI AWABARIKI MASHABIKI ZAKE NA THE JUICE BAR 3 ALBUM

RAPPER BARACK JACUZZI AWABARIKI MASHABIKI ZAKE NA THE JUICE BAR 3 ALBUM

Rapa kutoka nchini Kenya Barack Jacuzzi ameachia rasmi album yake mpya “The Juice Bar 3” ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

The Juice Bar 3 ina jumla ya ngoma saba za moto huku ikiwa na collabo 6 kutoka kwa wakali kama Bien Baraza, Scar Mkadinali, Camp Mulla, Boutrous na wengine wengi.

Album hiyo ambayo ina ngoma kama Rastaman, Want you Back, Friday Night, Nairobi inapatikana exclusive kwenye digital platform zote za kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni kama vie Boomplay Kenya na Spotify.

The Juice Bar 3 ni sehemu ya tatu ya Extended Playlist yake ya kwanza “The Juice Bar’ iliyotoka mwaka wa 2017.

Sehemu ya Pili ya EP hiyo ilitoka mwaka wa 2019 kama album ya kwanza kwa rapa Barack Jacuzzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke