Habari nzuri kwa mashabiki wa muziki nchini ni kwamba tutarajie muda wowote ujio wa Collabo kati ya mejja na Rapper Breeder LW.
Breeder LW amethibitisha taarifa hiyo kwa mashabiki kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram ambapo ameshare clip fupi ikimuonyesha akiwa location na mejja wakishoot video ya wimbo wao mpya ambayo kwa mujibu wake ni moto wa kuotea mbali.
Hata hivyo mashabiki maonekana kuikubali ngoma hiyo ambapo wamemtaka rapa Breeder lw kuaharakisha mchakato wa kuachia audio pamoja na Video.
Iwapo Breeder Lw na Mejja wataachia collabo yao hiyo itakuwa ni kazi yao ya kwanza kufanya kama wasanii wawili ikizingatiwa kuwa kipindi cha nyuma wamekuwa wakikutana kwenye kazi za wasanii wengine.