You are currently viewing RAPPER GRAVITY OMUTUJJU AKIRI HADHARANI KUACHA MUZIKI KWA AJILI YA KUINGIA KIFUA NDOA YAKE

RAPPER GRAVITY OMUTUJJU AKIRI HADHARANI KUACHA MUZIKI KWA AJILI YA KUINGIA KIFUA NDOA YAKE

Rapper asiyeishiwa na vituko kila leo kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju amekiri kuwa ni heri aache muziki badala kumpa talaka mke wake.

Akizungumza kuhusu familia yake katika mahojiano yake ya hivi karibuni Omutujju amesema anathimini sana mke wake na hawezi kumfanyia kitu kibaya kitakacho muumiza kiasaikolojia.

Hitmaker huyo wa ngoma “Tusimbudde” amesema Mke wake alisamama nae kipindi chote alichokuwa amevulia kiuchumi hivyo ni vigumu kwake kumsaliti kutokana na kujitolea kwake kuhakikisha familia yake inasimama imara licha ya changamoto ya maisha.

Hata hivyo amesema mewekeza pesa zake nyingi kwenye biashara ya ujenzi wa nyumba na shughuli zingine kuhakikisha ana ana kitega uchumi cha kustosha kwa ajili ya familia yake katika siku za usoni ambapo pia amedokeza mpango wake wa kuhalalisha ndoa yake hivi karibuni pindi tu atakapopata kipato kizuri.

Utakumbuka Gravity Omutujju na mke wake Sharua Nakanyike wamekuwa kwenye ndoa tangu mwaka wa 2013 na wamejaliwa watoto watatu kwa pamoja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke