Rapper Juliani ameripotiwa kufunga ndoa ya kimya kimya na mchumba wake Lilian Ng’ang’a baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda.
Kulingana na wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii,Harusi hiyo ambayo inadaiwa kuwa ya siri imiefanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na watu wachache wakiwemo wanafamilia pamoja na marafiki.
Mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamiii wameonekana kufurahia hatua ya wawili hao kuhalalisha mahusiano yao huku wengine wakiwa na mshangao kwanini ndoa hiyo imekuwa ya siri.
Hata hivyo Juliani na Lilian ng’ang’a hawajathibitisha chochote kuhusiana ndoa yao hiyo ila ni jambo la kusubiriwa.
Uhusiano wa kimapenzi kati ya rrapa Juliani na Lilian Ng’ang’a ulianza mapema mwaka jana , huku Juliani akithibitisha mahusiano hayo rasmi baada ya ukaribu wake na mrembo huyo gumzo mtandaoni ambapo wengi walishangazwa na hatua ya msanii huyo kutoka kimapenzi na Lilian Ng’ang’a ikizingatiwa alikuwa mke wa Gavana wa Machakos Alfred Mutua.
Ikumbukwe Agosti 15 mwaka 2021 Gavana Mutua na aliyekuwa mke wake Lilian nganga walitumia mitandao yao ya kijamii kuweka wazi kwamba hawapo tena pamoja hii ni baada ya ndoa yao kuvunjika miezi miwili iliyopita.