Rapper kutoka Kenya Kahush ameipuzilia mbali tamasha la “Most Wanted” ambalo litawaleta nchini wasanii wa kundi la Wstrn kutoka nchini Uingereza Aprili 22 mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram kahush amesema tamasha hilo ni batili huku akiwajia juu waandaji wa show hiyo kwa kutumia chapa yake ya “Most Wanted” bila idhini yake.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mastingo” amewataka mashabiki zake kususia tamasha hilo kwani lebo yake ya “Most Wanted” haijahusiki kivyovyote kuandaa show hiyo.Hata hivyo amesema madhumuni ya yeye kuja chapa ya “Most Wanted” ilikuwa ni kwa ajili ya kuwasaidia vijana na wasanii wa Kenya kukuza vipaji vyao kupitia muziki.