You are currently viewing RAPPER KHALIGRAPH JONES MBIONI KUACHIA WIMBO WA INJILI

RAPPER KHALIGRAPH JONES MBIONI KUACHIA WIMBO WA INJILI

Rapper mnoma kwa michuano kutoka Kenya Khaligraph Jones huenda akageukia muziki wa injili baada ya kushare video clip ikimuonesha akiimba na kutayarisha wimbo wa dini.

Hata hivyo rapper huyo ambaye amewahi kutamba na hitSong kama “Mazishi, Leave Me Alone, na Yes bana”  anatajwa kulelewa kwenye misingi thabiti ya dini ya Kikristo na mpaka sasa mama yake ni mhubiri.

Kwenye moja ya mahojiano yake Khaligraph Jones amewahi kuthibitisha kuwa Mwaka 2004, alikuwa na matarajio ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili, lakini yote yalibadilika mara baada ya kugundua uwezo wake wa kurap mwaka huo alirekodi wimbo wake wa kwanza pamoja na Hope Kid na walianzisha kikundi.

“Nilitaka kufanya kitu ambacho nilitaka kufanya na sio kufanya kwa sababu ya ushawishi. Nilitaka kujitengenezea njia yangu.Wakati huo nilikotoka, kila mtu ambaye alikuwa msanii alikuwa anafanya injili, lakini sikuwa na raha”  alisema Khaligraph Jones.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke