Rapa kutoka nchini Marekani Travis Scott pamoja na kampuni ya Live Nation wako matatani baada ya kesi takribani 400 kufunguliwa dhidi yao.
Kesi hizo zote zimeunganishwa kuwa kesi moja kubwa itakayowakilisha wahanga takribani 2,800 walioathirika na tukio la Novemba 5, mwaka wa 2021 ambapo ajali ilitokea kwenye tamasha la Astroworld.
Watu 10 walifariki na mamia kujeruhiwa baada ya kutokea msongamano mkubwa kipindi Travis scott alipokuwa anatumbuiza huko NRG park, Houston Texas nchini marekani.