Rapa kutoka Marekani Lil Durk amewapa tahadhari wasanii wanzake ambao nao wanamipango ya kuachia kazi zao mpya ijumaa ya wiki hii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram rapa huyo ambaye ni mzaliwa wa Chicago, Illinois ameweka wazi kuwa album yake ya “7220” haita ahirishwa tena na yeyote atakayetaka kuachia album yake Machi 11 mwaka huu ajipange kwa kuwa amejipanga kuuza zaidi ya wote watakaoachia album siku hiyo
Hayo yanajiri ikiwa ni wiki kadhaa zimepita tangu asogeze mbele tarehe ya kuachia album yake mpya iitwayo “7220” ambayo ilikuwa itoke Februari 22, tarehe moja na album ya Kanye West, akakubali yaishe akasogeza mbele album yake.