Msanii wa Hip Hop kutoka tanzania, Moni Centrozone ameachia rasmi Extended Playlist (EP) yake mpya inayokwenda kwa jina la Road To Mazengo.
EP hiyo ina nyimbo tano alizowashirikisha wasanii watano ambao ni Young Lunya, Slimsal, One Six na wengine wengi.
Maproduza waliohusika kutayarisha EP hiyo ni S2kizzy, Trakks, Slimsal, Pol Maker na Tony Drizy.
Utakumbuka EP hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Moni Centrozone inatoka chini lebo ya muziki ya RoofTop Entertainment.