Rapa mwenye utata nchini Tanzania Nay wa Mitego amewashutumu watumishi wa Mungu Masanja Mkandamizaji, Mc Pilipili na Nabii Shilla kuwa ni manabii wa uongo ambao kwenye vitabu vya dini wameandikwa.
Kupitia Instastory yake kweny mtandao wa Instagram Nay wa Mitego ameandika ujumbe unaosomeka “Mimi ndio maana sitakagu aya mambo ya Dini sijui nini.Yani Din imekuwa biashara hulia, eti Masanja Nae Mchungaji kuna mwingine yule tapeli Shilla sijui pumbavu kabisa. Huu ndio ule mwisho wa dunia ulioandikwa kwenye vitabu. Manabii wa uongo wamekuwa wengi mno”.
Masanja na Mc Pilipili ni kati ya wachungaji waliotokea kwenye tasnia ya uchekeshaji na baadae kutangaza kumtumia Mungu kwa kufungua makanisa yao