Rapa NLE Choppa kutoka nchini Marekani wamerushiana makonde na shabiki wa rapa NBA YoungBoy baada ya kuingia kwenye ugomvi wakiwa uwanja wa ndege.
Inasemekana kuwa ngumi ya kichwa na ya shingo vilitosha kumuangusha chini shabiki huyo ambaye alibamiza kichwa chini baada ya kuanguka na kulala hapo hapo.
Sababu ya ugomvi huo inasemekana kuwa ni baada ya NLE Choppa kufanya moja ya interview hivi karibuni na kusema kwamba hapo awali nba young boy alikuwa moja kati ya wasanii wake anaowakubali zaidi lakini kutokana na ngoma yake mpya “Bring the Hook” aliyowa-diss genge la kihalifu la O’block na marehemu King Von ameamua kumkataa