You are currently viewing RAPPER NOTI FLOW AMZAWADI MPENZI WAKE KING ALAMI GARI JIPYA

RAPPER NOTI FLOW AMZAWADI MPENZI WAKE KING ALAMI GARI JIPYA

Female rapper kutoka Kenya Noti Flow ameamua kutoonyesha zawadi ambayo amemnunullia mpenzi wake mwanadada King Alami wakati huu anaelekea kusherekea kumbukizi ya kuzaliwa kwake, Machi 25.

Kupitia ukarasa wake wa Instagram Hitmaker huyo wa ngoma ya “Photo Moto” ametusanua kwamba amemzawadi mpenzi wake King Alami gari jipya yenye thamani ya shillingi millioni 1.5 kutokana na upendo wa dhati alionao kwa mrembo huyo.

Noti flow ameenda mbali na kutoa ya moyoni kwa kusema kwamba licha ya wanaume kumtesa kihisia kiasi cha kumfanya kukata tamaa kwenye ishu ya mapenzi, King Alami alimsahulisha machungu yote kwa kumpa mahaba mazito.

Utakumbuka Noti Flow na King Alami walihalalisha mahusiano yao mwaka wa 2019 ambapo alienda mbali zaidi na kutangazia umma kuwa amejiunga na jamii ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke