Rapa Kutoka Nchini Marekani Young Thug ameonesha kuwa na moyo wa uhuruma baada ya kuguswa na kitendo cha Watu weusi nchini Ukraine kuachwa vitani huku wazungu wakisafirishwa sehemu salama zaidi.
Kitendo hicho cha kibaguzi kimemgusa Rapa Young Thug ambaye amejitokeza na kusema kuwa yupo tayari kutoa msaadakwa Waafrika waliokwama kuondoka Ukraine kipindi hichi cha vita na Urusi.
Hata hivyo amewaomba marapa wengine kushirikiana kufanikisha hilo huku akizitaka familia za waafrika waliokwama nchini Ukraine kumcheki kwa kuwa taratibu za kuondoka nchini humo kwa sasa ni ngumu.