You are currently viewing RASMI: NICCAH THE QUEEN ATHIBITISHA KUACHANA NA DJ SLAHVER

RASMI: NICCAH THE QUEEN ATHIBITISHA KUACHANA NA DJ SLAHVER

Msanii wa nyimbo za injili nchini Niccah The Queen ameweka wazi kuwa yeye na mchumba wake DJ Slahver wameachana.

Niccah amebainisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema amechukua maamuzi ya kuachana na mpenzi wake huyo baada ya kuafikia makubaliano ya pamoja huku akimtakia kila la kheri kwenye maisha yake mpya.

Hata hivyo Niccah The Queen hajatoa maelezo zaidi kuhusu kiini cha uhusiano wake na DJ Slahver kuvunjika  ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda msanii huyo anatengeza  mazingira ya kumzungumziwa nchini Kenya kabla ya ujio wa ngoma yake mpya

Ikumbukwe kuwa penzi la Niccah The Queen na DJ Slahver lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Dkt. Ofweneke.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke