You are currently viewing RAY C ACHUKIZWA NA KITENDO CHA DIAMOND KUZOMEWA MAREKANI

RAY C ACHUKIZWA NA KITENDO CHA DIAMOND KUZOMEWA MAREKANI

Mara baada ya kuwepo kwa kile kinachoonekana ni kubezana kwa watu waliokaribu na Diamond Platnumz na Harmonize kufuatia show za wasanii hao nchini Marekani, Mkongwe wa Bongofleva, Ray C ametaja huo kama Ulimbukeni.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Ray C amesema kwamba kumbeza harmonize na diamond kutokana shows zao za nchini marekani sio sawa kwani itakuwa vigumu kwa wasanii wa bongo kushindana na wasanii wa nchi nyingine kama Nigeria kwa mtindo huo.

Hitmaker huyo wa “Mapenzi yangu” amesema watu waache suala la kumshindanisha harmonize na diamond platinumz  na badala yake wajivunie namna wasanii hao wanavyoiwakilisha vyema nchi ya tanzania kimataifa kupitia kazi zao za muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke