You are currently viewing RAY C AOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI SAKATA LA DIAMOND NA HARMONIZE

RAY C AOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI SAKATA LA DIAMOND NA HARMONIZE

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Ray C ametia neno kuhusu bifu ya Harmonize na Diamond platinumz kwa kusema kwamba ugomvi wa wawili hao usipotatuliwa mapema unaweza kuwa mbaya.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Ray C amesema Watanzania hawapaswi kufurahia jambo hilo kama kweli wanawapenda wasanii hao ikizingatiwa kuwa ni vita kubwa sana ya kuharibiana Brand.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anaishi Ufaransa,  amewaomba viongozi wa serikali nchini Tanzania kuingilia kati na kutatua tofauti ambazo zipo kati ya wawili hao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke