Mwanamuziki Ray G amefunguka sababu za kutokuwa mwanachama wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Msanii huyo amesema chama hicho hakina mweelekeo lakini pia hajashawishika namna inawasaidia wasanii.
Ray G ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Nobanza” amedai kwa sasa ana mpango wa kujiunga na UMA hadi pale atakapopata mwanga ya jinsi inatekeleza majukumu yake.
Chama cha UMA katiika siku za hivi karibu kimepata pingamizi kutoka kwa wanamuziki mbali mbali nchini Uganda wengi wakidai kuwa hawaoni umuhimu wa chama hicho kwa kuwa imeshindwa kutetea maslahi ya wasanii.