Hatimaye msanii wa bongofleva Rayvanny amekata kiu ya mashabiki zake na Ep mpya inayokwenda kwa jina la Unplugged Session.
Rayvanny ameamua kuwa surprise mashabiki zake kwa kuachia Extended Playlist hiyo mpya yenye jumla ya mikwaju 8 ya moto huku ikiwa na kolabo moja pekee kutoka msanii aitwaye Fari.
Unplugged Session EP ina nyimbo kama Mama, Vacation, I Love You, Mwamba, Mtoto na nyingine nyingi.
Hata hivyo Rayvanny kupitia mitandao yake ya kijamii amesema ameachia Unplugged Session EP kama zawadi ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.
EP hiyo kwa sasa inapatikana exclusive kwenye Digital Platforms zote za kusambaza muziki duniani ikiwemo Boomplay.