Kuizuia nyota ya Rayvanny ni sawa na kuziba mwanga kwa kiganja cha mkono. Staa huyo wa muziki nchini tanzania na bosi wa lebo ya Next Level Music, ameingia kwenye chati za Billboard Latin.
Hii ni baada ya wimbo wa “Mama Tetema” aliyoshirikishwa na Maluma, staa wa muziki kutoka Colombia kuingia kwenye chati hizo kubwa, na kukamata namba 12.
Wimbo wa Mama Tetema wake wa Maluma unazidi kumfungulia njia Rayvanny kimataifa zaidi kwani ni wiki mbili zimepita tangu atumbuize wimbo huo kwenye hafla ya tuzo za MTV EMA.
Hata hivyo Rayvanny anakuwa msanii wa kwanza nchini Tanzania kuingia kwenye chati za Billboard Latin, lakini pia inakuwa mara yake ya pili kuingia kwenye chati za Billboard.
Aliwahi kuingia kwenye chati za Billboard kupitia kolabo na Dj Cappy kutoka Nigeria, kwani wimbo wao uitwao “Jollof On The Jet” uliingia kwenye chati za Top Triller Global mwaka wa 2020