You are currently viewing RAYVANNY ADOKEZA UJIO WA KOLABO YAKE NA KAYUMBA

RAYVANNY ADOKEZA UJIO WA KOLABO YAKE NA KAYUMBA

Staa wa muziki wa Bongofleva, msanii Rayvanny ambaye aliweka wazi kusaidia wasanii wenye vipaji kutoka ndani na nje ya tanzania, hatimaye ameweza kulitekeleza hilo.

Boss huyo wa Next Level Music kupitia insta story yake, ametangaza kukamilika kwa kolabo yake na msanii Kayumba, na ameutaja wimbo huo kuwa wimbo bora Afrika.

Kayumba ambaye amekuwa na muendelezo wa kufanya kazi nzuri, kwa sasa ana EP yake mpya iitwayo “Sweet Pain” ambayo inazaidi ya streams laki 500 BoomPlay.

Hii inaenda kuwa kolabo ya NNE kwa mtu mzima Kayumba kufanya na wasanii wa Tanzania. Tayari ana kolabo na Linah, Isha Mashauzi na Marioo.

Hata hivyo, Rayvanny anafanya kile alichowahi kukieleza siku za nyuma kwamba anatamani wasanii wa Tanzania kushirikiana katika kuupeleka muziki wa bongofleva kimataifa zaidi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke