Mwanamuziki wa Bongofleva Rayvanny ni kama amejibu yanaendelea mitandaoni kuhusu kupigwa faini ya shilling million 2 za Kenya na lebo yake ya zamani WCB.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Rayvanny amechapisha ujumbe unao wajulisha watu wake kuwa yeye ni msanii anayejitegemea na yupo katika management nyingine kama alivyo weka utambulisho wake katika mtandao wa instagram.
“Hellow my people RAYVANNY ni independent artist ,chek my new management for all bookings details on my bio” ameandika Rayvanny
Kwa mujibu wa taarifa zinazoendelea kushika kasi kwa sasa mtandaoni zinaeleza kuwa mwanamuziki ambaye anatajwa kutoka kwenye record label ya WcB Wasafi Rayvanny amekumbana na faini ya shilling million 2 kutoka WCB kwa kukiuka sheria na kanuni za mkataba.
Taarifa zinadai kuwa sababu kubwa ni kitendo cha mwanamuziki huyo kuhudhuria tamasha la mwanamuziki mwenzake Nandy “Nandy Festival” mapema mwezi uliopita mkoani Ruvuma nchini Tanzania, kabla ya kukamilisha masharti yote ya kujitoa katika record label hiyo ya WcB Wasafi ikiwemo kulipa kiasi cha zaidi ya Million 40 za Kenya.