You are currently viewing Rayvanny akiri kukua kisanaa tangu aondoke WCB

Rayvanny akiri kukua kisanaa tangu aondoke WCB

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Rayvanny amesema tangu aondoke kwenye Label ya WCB amejihisi kukua Kimuziki na kwa sasa anawaza mambo makubwa zaidi.

Akizungumza na mtandao wa Habari Leo, amesema changamoto anazokutana nazo pamoja na ushindani uliopo kwenye game ya bongo fleva, vimemkomaza zaidi.

“Ukweli sijutii maamuzi yangu, zaidi napambana ili niweze kuwa mkubwa zaidi, sababu huku kila kitu wakuulizwa ni Mimi na sababu ndio Boss mkubwa ninayehusika na mambo yote ikiwemo kulipa wasanii na mengineyo.” amesema Rayvanny.

Aidha amesema kwa jinsi anavyofanya vizuri katika game hiyo, anaamini mpaka kufikia mwaka ujao atakuwa miongoni mwa wasanii wakubwa nchini na wenye wafuasi wengi kuliko ilivyo hivi sasa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke