Nyota wa muziki nchini Tanzania, msanii Rayvanny amefunguka namna anavyoumizwa na kuchomwa kwa vitu kwenye video zake, na sasa ametoa agizo kwa director wake Eris Mzava kutoweka scene za namna hiyo kwenye video za nyimbo zake.
Rayvanny amebainisha hilo kupitia insta story yake ambapo ameteketeza kwa moto gari aina ya Alteza kwenye video yake mpya ya wimbo wa ” Te Quiero” aliyomshirikisha Marioo.
“Najua kweli ni uhalisia lakini hakuna scene imeniumiza moyo kama scene ya kuchoma gari. Director Mzava naomba tuishie hapa kuchoma choma vitu” ameandika Rayvanny Instagram.
Ikumbukwe, hii inakuwa mara ya pili kwa boss huyo wa Next Level Music kuteketeza vitu kwa moto kupitia video zake huku akitumia gharama kubwa katika uandaaji.