Nyota wa muziki wa Bongofleva, Rayvanny amedai kuwa video ya wimbo wake, “I Miss You” ambayo ndio video yenye gharama kubwa zaidi miongoni mwa zile ambazo zimetengenezwa nchini Tanzania.
Boss huyo wa Next Level Music (NLM) amesema hayo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram ambapo ameeleza, ametumia kipindi cha miezi mitatu hadi video ya wimbo huo aliyomshirikisha Zuchu kukamilika.
Akifafanua zaidi kuhusu scene 3 za nguvu za video hiyo, Rayvanny amesema scene ya helikopta iliwatesa sana kwani kila ilipokuwa ikiruka iliwabidi kulipia kwani imeshutiwa vipande zaidi ya kimoja.
Scene ya nyumba amesema ilibidi watengeneze nyumba na baada ya shughuli kuisha wakaichoma moto na Scene ya Train ameitaja kuwa pesa imetumika sana